Al-Qaeda

al-Qaeda
القاعدة
Bendera ya Al-Qaeda.
Dates of operation1988–sasa
LeaderAyman al-Zawahiri
Active region(s)Dunia
IdeologyKiislamu
Islamic fundamentalism
Sunni Islam[1]
Pan-Islamism
Salafi
Qutbism
StatusDesignated as Foreign Terrorist Organization by the U.S. State Department[2]
Designated as Proscribed Group by the UK Home Office[3]
Designated as terrorist group by EU Common Foreign and Security Policy[4]

Al-Qaeda (pengine imeandikwa al-Qaida; kutoka Kiarabu al-qa'idah, "msingi") ni kundi la Kiislamu lililoanzishwa kati ya Agosti 1988 [5] na mwanzoni mwa 1990. [6]

Ni mtandao wa kimataifa usiotegemea taifa fulani[7] na kundi la wanaharakati wa Sunni wanaotoa wito wa jihad kwa ulimwengu mzima.

Al-Qaeda imeweza kushambulia raia na malengo ya kijeshi katika nchi mbalimbali, mashuhuri zaidi ikiwa mashambulio ya 11 Septemba 2001. Serikali ya Marekani iliitikia kwa kuzindua Vita dhidi ya Ugaidi. Kati ya wanachama 3,000 na 4,000 wa mtandao huu wamekamatwa, na maelfu zaidi kuuawa vitani Afghanistan.

Mbinu zao za kushambulia ni pamoja na mashambulizi ya kujitolea mhanga na ulipuaji wa mabomu ya malengo tofauti kwa wakati mmoja. [8] Shughuli zake zinaweza kuhusisha wanachama wa harakati, ambao wamechukua amana ya uaminifu kwa kiongozi (sasa Mmisri Ayman al-Zawahiri), au wengi zaidi "watu binafsi wanaohusishwa na al-Qaeda" ambao wamepitia mafunzo katika moja ya kambi zake nchini Afghanistan au Sudan, bila kuchukuliwa amana yoyote. [9]

Wakereketwa wa Al-Qaeda wanaangazia kukatiza kabisa mvuto wa kigeni katika nchi za Kiislamu, na uumbaji wa ahmadiyya mpya ya Kiislamu. Imani ambazo zimeripotiwa ni pamoja na kuwa muungano wa Wakristo na Wayahudi unakusudia kuharibu Uislamu, [10] na kwamba mauaji ya raia wanaopatikana pahali pa mashambulizi yanakubalika katika jihad.

Usimamizi wake falsafa umeelezewa kama "umoja wa uamuzi na madaraka ya utekelezaji mikoani." [11] Kufuatia vita dhidi ya ugaidi, imedhaniwa kwamba uongozi wa al-Qaida "umegawanyika kijiografia", na hili limepelekea "kuibuka kwa uongozi uliogawanywa kikanda" wa makundi yanayotumia jina la al-Qaeda.

  1. Atwan 2006, p. 40.
  2. "Foreign Terrorist Organizations List". United States Department of State. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2002-10-02. Iliwekwa mnamo 2007-08-03.USSD Foreign Terrorist Organization
  3. "Terrorism Act 2000". Home Office. Iliwekwa mnamo 2007-08-14.Terrorism Act 2000
  4. "Council Decision". Council of the European Union. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2005-05-06. Iliwekwa mnamo 2007-08-14.
  5. Bergen 2006, p. 75
  6. United States District Court, Southern District of New York (6 Februari 2001). "Testimony of Jamal Ahmad Al-Fadl". United States v. Usama bin Laden et al., defendants. James Martin Center for Nonproliferation Studies. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2001-12-14. Iliwekwa mnamo 2008-09-03.
  7. Gunaratna 2002, pp. 95–96. "Mtandao wa kimataifa wa Al Qaida, tunavyoijua leo, iliundwa mjini Khartoum, kuanzia Desemba 1991 hadi Mei 1996. Ili kuratibu oparesheni zake wakati makadirio na rasilimali zake zikiongezeka,iliunda uongozi wa kikanda. [...] Kama mtandao wa kimataifa, Al Qaeda hufanya mataifa na makabila tanzu, ambapo kuna dazeni kadhaa, kuwajibika kwa kanda au eneo la kijiografia fulani. Ingawa modus operandi yake ni ya seli, mahusiano ya kifamilia yanahimili."
    Tazama pia:
    • Naím. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help); Missing or empty |title= (help); Unknown parameter |kichwa= ignored (help); Unknown parameter |kurasa= ignored (help); Unknown parameter |kwanza= ignored (help); Unknown parameter |nakala= ignored (help); Unknown parameter |tarehe= ignored (help); Unknown parameter |toleo= ignored (help)
  8. Wright 2006, pp. 107–108, 185, 270–271
  9. Wright 2006, p. 270
  10. Fu'ad Husayn `Al-Zarqawi ... "The Second Generation of al-Qaida, Sehemu ya Kumi na nne," Al-Quds al-Arabi, 13 Julai 2005
  11. al-Hammadi, Khalid, `The Inside Story of al-Qaeda,` sehemu ya 4, Al-Quds al-Arabi, 22 Machi 2005

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search